Sunday, 20 November 2016

Walter Chilambo wa gospel ni hatari ya ulivyokuwa ukimjua

Ni swali ambalo wengi hujiuliza na wasipate majibu ya kuridhisha, kwamba kwanini washindi wa Bongo Star Search huwa hawafanikiwi? Inashangaza sababu uwezo wao wawapo kwenye shindano hilo huwa mara mbili zaidi ya wasanii maarufu wanaofanya vizuri, lakini wakishaingia tu mtaani hushindwa kufanya muziki wa maana.

Licha ya kuwa mmoja wa waimbaji bora kuwahi kutokea, Walter Chilambo aliyeshinda shindano hilo mwaka 2012, naye alijikuta akisombwa na upepo huo. Ilifikia wakati Walter aliacha kuachia nyimbo mpya na kufanya tu cover hali iliyowafanya baadhi ya watu kudhani kuwa ameishiwa.
Kumbe muimbaji huyu kutoka Mbeya alikuwa ni kama kobe aliyeinama akitunga sheria na kutafakari njia nzuri ya kurejea kuonesha uwezo wake. Ukimya wake ulimsaidia kuutambua muziki anaoweza kufanya na kupata heshima anayostahili.
Walter ameamua kuimba muziki wa injili na kwa wimbo wake Asante, ni dhahiri amedhamiria kuja kuokota kila senti aliyopaswa kuikota tangu kitambo. Asante ni wimbo unaotoa tafsiri ya muziki wa injili wa kisasa. Ni wimbo mtamu, wenye hisia na utunzi unaoweza kukutoa vinyweleo vya baridi kwa msisimko.
Ni utunzi wa aina yake unaofungua ukurasa mpya wenye kila dalili ya mafanikio makubwa. Asante ina video safi inayoendana na ukubwa wimbo wake na kwa waumini wa dini ya kikristo wimbo huu una nafasi ya kuwa maarufu kwenye playlist zao. Sasa muimbaji huyo anajiweka kwenye ligi moja na Gudluck Gosbert – muimbaji mwingine mahiri wa gospel ya kisasa. Anaongeza idadi ya waimbaji wa muziki wa injili wanaoweza kuipa Tanzania sifa nyingine kama ambavyo wasanii kama Diamond, Alikiba, Vanessa Mdee na wengine wanaipa katika muziki wa Bongo Flava. Kwa alichokifanya Walter ni kama kujivua gamba na kurudi upya katika muziki ambao kwa sasa si kama huduma tu, bali biashara kama tu muziki wa kidunia ulivyo.

Barnaba awataka wasanii wanaofanya muziki wa kubahatisha watafute kazi nyingine

Hitmaker wa ‘Lover Boy’ Barnaba amewataka wasanii wanaofanya muziki kwa kubahatisha wabadilike au watafute kazi nyingine.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One kuwa muziki unapoelekea kwa sasa ni mgumu na hakuna shabiki anayeweza kuongopewa kwa kuwa wanafahamu anafanya muziki mzuri na anayebahatisha.
“Wajitathimini wale wanaofanya muziki mzuri na muziki mbovu, wale wanaofanya muziki mzuri waongeze tu creativity. Wale wanaofanya muziki ambao hauishi nawashauri waache tu kwa sababu dunia tunayoenda hakuna ‘uongo uongo’ na mashabiki wanajua nani anafanya vizuri na nani anafanya vibaya na hakuna wakumdanganya utakuwa unajidanganya mwenyewe. Nashauri kila mtu aendelee kujituma hakuna uongo, hakuna mtu anayefanya uongo, hakuna mtu anayetaka kuongopewa,”amesema Barnaba.
Barnaba ameongeza kuwa wasanii waache kupoteza muda mwingi kwenye kutengeneza video pekee wafanye hivyo mpaka kwenye audio kuhakikisha zinakuwa nzuri pia.

Majani adhamiria kumrudisha Cpwaa kwenye chati

Producer mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya Bongo Flava, P-Funk Majani anasema ‘mwenye muziki wake anarudi.’ Na kwakuwa tunajua ni hits nyingi kiasi gani zilizotoka kwenye studio yake ya Bongo Records, hiyo si kauli tunayoweza kuitilia mashaka.

Miezi ya hivi karibuni Majani ameonekana kutumia muda mwingi zaidi kwenye studio yake kutengeneza nyimbo mpya. Miongoni mwa kazi anazozipika ni za rapper Cpwaa ambaye amekuwa kimya kwa takriban miaka miwili na kitu sasa.
Producer huyo ameapa kumrudisha tena kwenye chati rapper huyo aliyewahi kuhit na nyimbo kama Problem, 6 In The Morning, Action na zingine.
“Day 2 @cpwaa nailed it! This boy got No chill, I am bringing him back! Stay tuned #BongoRecords #DreamBig #KiumeniSoundTracks #MwenyeMzikiWakeAmerudi,” aliandika Majani kwenye Instagram hivi karibuni.
Naye Cpwaa amemuelezea Majani kama kaka na mwalimu wake na kwamba kufanya kazi naye tena ni heshima kubwa. “Again it was a good day! #BongoRecords PFunk @majani187 #TheGodFatherOfBongoFlavaMusic is more than a Music Producer! He is a Mentor, a Brother, and Family. Before the session we went through a lot of ongoing main stream shiit, this brother is doing his homework.i keep learning everyday from him #Discpline is number 1thing when it comes to work with him.#TheComeBackOfCpwaa.”

Karibu djyusto.blogspot.com kwa story za burudani unakaribishwa sana

kwa mega mix kali subiri kidogooooooo utajuzwa nini cha kufanya.........